KITABU CHA DARASA LA KWANZA
YALIYOMO
UTANGULIZI
Sura ya
Kwanza: Kutambua dhana ya namba
Sura ya
Pili: Kutumia matendo katika namba
Sura ya
Tatu: Kutambua uhusiano wa vitu na namba
Sura ya
Nne: Kutambua vipimo
Sura ya
Tano: Kutambua maumbo
Sura ya
Sita: Kukusanya na kuorodhesha vitu

Kitabu hiki kimezigatia muongozo wa
utoaji wa vitabu,
wa mwaka 2018 toleo la kwanza.
UTANGULIZI
Hiki
ni kitabu cha pili cha mwanafunzi wa shule ya msingi. Ni kitabu kilichobeba
misingi mbalimbali ya hisabati na kimezingatia mtaala wa utungaji wa vitabu wa
mwaka 2018 toleo la kwanza, na maanisha kuwa mada zote zilizopo kwenye kitabu
hiki zimezingatia mtaala wa kitaifa.
Kitabu hiki kimebeba
mada zifuatazo; Kutambua dhana ya namba,Kutumia matendo
katika nambo,Kutambua uhusiano wa vitu na namba,Kutambua vipimo,Kutambua
maumbo,Kukusanya na kuorodhesha vitu. Ni mada zitakazomwongoza mwanafunzi
wa darasa la pili kufaulu mitihani yake katika somo la hisabati. Kina
mazoezi ya kutosha ya kumuwezesha mwanafunzi kujijengea uwezo wa kujifunza
hesabu kwa undani zaidi. Ni matumaini yetu kuwa kitabu hiki kitakuwa msaada kwa
mwanafunzi wa ngazi hii. Mbali na kitabu hiki Joakim Work Production
tumekuandalia vitabu vingine mbalimbali kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka
ngazi ya kidato cha sita kama vinavyoonekana katika picha zifuatazo hapo chini.
|

|
Joakim work production
All Springs of your success are here
Sura ya Kwanza
Kutambua dhana ya namba
Karibu katika sura hii
ya maudhui ya kuhesabu inayolenga kukujengea umahiri katika kumwezesha
mwanafunzi kutambua dhana ya namba kwa usahihi. Wakati wa kujifunza sura hii
mahususi, utaboresha ufundishaji wa dhana ya namba, msamiati wa namba, kusoma,
kuhesabu na kuandika namba kwa ufanisi. Katika ngazi ya darasa la pili mwanafunzi
anapaswa kujifunza kuandika na kuhesabu kuanzia moja mpaka mia moja.
Mfano: 1- hii ni moja
10 – Hii ni kumi
100 – Hii ni miamoja
Kwa kurahisisha tazama
nafasi zifuatazo za namba
|
namba |
Nafasi ya namba |
||
|
|
mamia |
makumi |
mamoja |
|
1 |
- |
- |
1 |
|
10 |
- |
1 |
0 |
|
90 |
- |
9 |
0 |
|
88 |
- |
8 |
8 |
|
100 |
1 |
0 |
0 |
Kila namba ina nafasi
yake kama vile namba moja ina nafasi
moja nayo ni mamoja pekee, kumi ina nafasi mbili nazo ni kama ifuatavyo: nafasi ya mamoja na nafasi ya makumi na mia moja ina nafasi tatu nazo mamoja, makumi na mamia.
|
![]() |
||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||
Kufafanua dhana
ya namba
Karibu
katika sehemu hii ya kwanza ya kutambua dhana ya namba inayolenga kukujengea
umahiri zaidi katika kumfundisha mwanafunzi dhana ya namba. Katika sehemu hii utajifunza dhana ya namba
na kutambua wingi na uchache wa vitu.
Dhana ya namba:Namba ni alama inayowakilisha idadi ya vitu au
kipimo cha kiwango cha kitu.
Unapoanza kufundisha dhana ya namba ni muhimu kuanza kumfundisha mwanafunzi
kuhusianisha idadi ya vitu na namba nzima kama vile 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8 na
9. Dhana ya namba humsaidia mwanafunzi
katika kuhesabu vitu na kujenga msingi
mzuri wa ujifunzaji wa hisabati.
Je,
sifuri ni namba? Toa sababu.
Mfano wa sifuri: Ndege wawili walitua mtini. Baadae ndege mmoja
aliruka na kisha ndege wa pili aliruka. Je walibaki ndege wangapi? Jibu:
Hakubaki ndege hata moja.
Bila
shaka utakuwa unaelewa kuwa sifuri ni alama inayoashiria kutokuwepo kwa kitu.
Je, utamjengeaje mwanafunzi dhana ya sifuri?
Je, ni vifaa gani utavitumia katika kumjengea mwanafunzi dhana ya
sifuri?
Kutambua wingi na uchache wa vitu.

Chati
hii inaonesha vitu vingi na vitu vichache.
Kujenga msamiati wa namba
Katika kujenga msamiati wa namba
kwa wanafunzi unaweza kutumia mbinu mbalimbali kama vile nyimbo, michezo,
igizodhima na vitendo mbalimbali kwa kurudia rudia. Mfano wa wimbo unaoweza
kuutumia kujenga msamiati wa namba ni huu ufuatao:
Naweza kuhesabu namba! Moja, mbili, tatu x 2
Nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi! x 2
Vidole vya mikono yangu, jumla yake kumi! x 2
Huku tano na huku tano, jumla
yake kumi.x 2
Sura ya Pili
Kutumia matendo
katika namba
Karibu
katika sura ya pili inayohusu dhana ya matumizi ya matendo katika namba.
Utakapokuwa unajifunza sura hii, utajijengea umahiri wa matumizi ya matendo
katika namba na namna ya kumwezesha mwanafunzi kutumia matendo hayo.
Kwa
ngazi ya mwanafunzi wa darasa la pili kuna matendo matatu nayo ni kama
ifuatavyo;
·
Kujumlisha
·
Kutoa na
·
Kuzidisha
KUJUMLISHA
Kujumlisha ni kuongeza namba na katika ngazi hii ya
darasa la pili tutajifunza kujumlisha namba mpaka mia moja.
Kuna njia mbili za
kuzitumia wakati wakufanya hesabu za kujumlisha nazo ni: kujumlisha kwa wima na kujumlisha
kwa ulalo
Mfano: a. Kujumlisha kwa
ulalo
1.
10 + 10 = 20
2.
20 + 30 = 50
3.
30 + 10 =40
4.
30 + 5 = 35
b. Kujumlisha kwa wima
5. 10
+20
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
30
ZOEZI
Fanya zoezi lifuatalo kwa
kujumlisha kwa njia ya ulalo.
1.
20 +20 =
2.
15 +20 =
3.
12 + 12 =
4.
12 + 13 =
5.
10 + 15 =
6.
40
+ 10
7.
23
+13
8.
42
+
21
KUTOA
Kutoa ni kupunguza
namba, kama ilivyo kujumlisha kutoa pia kuna njia mbili nazo ni; kutoa kwa njia
ya ulalo na kutoa kwa njia ya wima. Katika ngazi hii tutapunguza namba kutoka
idadi ya miamoja.
Chunguza kwa umakini
mifano hii
|
1.
100- 50 = 50
2.
50 – 20 = 30
3.
|
20
– 10 = 10
4.
80 – 20 = 60
ZOEZI
Fanya zoezi lifuatalo
kwa njia ya kutoa ukitumia njia zote mbili yaani njia ya wima na ulalo.
1.
32 – 12 =
2.
34-
23=
3.
15- 10=
4.
17- 10=
5.
16 - 7=
6.
20 – 14 =
KUZIDISHA
Katika ngazi ya darasa la pili tuajifunza kuzidisha
kuanzia namba moja mpaka kumi.
Angalia mifano hii,
1x 1= 1
1x 2= 2
1x3= 3
Angalia mfano huu pia;
2x3 = 6
3x2 =6
Kwa
kifupi angalia chati hii
|
x |
1 |
2 |
3 |
4 |
5 |
6 |
7 |
8 |
9 |
10 |
11 |
12 |
|
|||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||||||
|
1 |
1 |
2 |
3 |
4 |
5 |
6 |
7 |
8 |
9 |
10 |
11 |
12 |
|
|||||
|
2 |
2 |
4 |
6 |
8 |
10 |
12 |
14 |
16 |
18 |
20 |
22 |
24 |
|
|||||
|
3 |
3 |
6 |
9 |
12 |
14 |
16 |
18 |
20 |
22 |
24 |
26 |
28 |
|
|||||
|
4 |
4 |
8 |
12 |
16 |
20 |
24 |
28 |
32 |
36 |
40 |
44 |
48 |
|
|||||
|
5 |
5 |
10 |
15 |
20 |
25 |
30 |
35 |
40 |
45 |
50 |
55 |
60 |
|
|||||
|
6 |
6 |
12 |
18 |
24 |
30 |
36 |
42 |
48 |
54 |
60 |
66 |
72 |
|
|||||
|
7 |
7 |
14 |
21 |
28 |
35 |
42 |
49 |
56 |
63 |
70 |
77 |
84 |
|
|||||
|
8 |
8 |
16 |
24 |
32 |
40 |
48 |
56 |
58 |
66 |
74 |
82 |
90 |
|
|||||
|
9 |
9 |
18 |
27 |
36 |
45 |
54 |
63 |
72 |
81 |
90 |
99 |
108 |
|
|||||
|
10 |
10 |
20 |
30 |
40 |
50 |
60 |
70 |
80 |
90 |
100 |
110 |
120 |
|
|||||
|
11 |
11 |
22 |
33 |
44 |
55 |
66 |
77 |
88 |
99 |
110 |
121 |
132 |
||||||
|
12 |
12 |
24 |
36 |
48 |
60 |
72 |
84 |
96 |
108 |
120 |
132 |
144 |
||||||
NB:
Pia hata kuzidisha kuna njia mbili nazo ni: kwa njia ya ulalo na njia ya wima.
MAZOEZI YA KUZIDISHA
Fanya
hasabu zifuatazo kwa kuzidisha
1.
1x 2=
2.
3x5=
3.
2x2=
4.
5x5=
5.
4x4=
6.
4x2=
7.
5x2=
Sura ya Tatu
Kutambua uhusiano wa vitu na namba
Karibu
katika sura hii inayolenga kukujengea umahiri katika kumfundisha mwanafunzi
uhusiano wa vitu na namba. Baada ya kujenga umahiri huu mahususi utamwezesha
mwanafunzi kujenga dhana ya sehemu na fedha za Tanzania.
Baada
ya kujifunza maudhui ya sura hii utajenga umahiri katika:
i.
dhana
ya sehemu.
ii.
fedha za Tanzania.
Dhana ya sehemu
Sehemu hii
inakufundisha namna ya kumwezesha mwanafunzi kusoma na kuonesha kwa vitendo
dhana ya sehemu na namna ya kumfundisha mwanafunzi kuandika sehemu kwa kutumia
namba.
Unatakiwa kuelewa uhusiano uliopo kati ya
sehemu na kitu kizima. Kitu kizima kikigawanywa katika vipande linganifu au
sawa, sehemu ni moja au zaidi ya vipande hivyo.
Sehemu za kawaida
huandikwa katika muundo huu: a /b
, mfano 1/ 2
, 1/ 4
na 1/ 3
.
a - inawakilisha kiasi
b - inawakilisha asili
Kiasi kinawakilisha
sehemu na asili inawakilisha kitu kizima.
Sasa
chunguza vielelezo vifuatavyo:

Dhana ya nusu, robo na theluthi
Uhusiano kati ya nusu,
robo na theluthi
![]() |

Fedha ya Tanzania
Wakati
wa kujifunza namna ya kumfundisha mwanafunzi dhana ya fedha za Kitanzania
unatakiwa kuwa na umahiri katika kutambua fedha za Tanzania na matumizi yake na
kulinganisha thamani ya sarafu na noti katika kufanya manunuzi ya bidhaa
mbalimbali. Pia, utajifunza namna bora ya kufundisha hesabu za kujumlisha na
kutoa fedha za kitanzania.
Fedha
ni noti au sarafu yenye thamani iliyokubalika katika nchi fulani inayotumika
katika kubadilishana vitu au malipo ya bidhaa na huduma. Unaweza kubadilishana
kile unachohitaji kwa thamani ya noti au sarafu uliyonayo.
Bila
fedha, bidhaa au huduma zingekuwa zinabadilishwa zenyewe kwa zenyewe. Hii ina
maana kwamba bidhaa fulani aliyonayo mfanyabiashara ni lazima ifanane au
ilingane kwa thamani na bidhaa nyingine.

Sarafu ya nchi
yetu ya Tanzania

Noti ya nchi yetu
Sura ya Nne
Kutambua vipimo
Karibu katika sura hii
inayohusu dhana ya kutambua vipimo. Sura hii itakuwezesha kujenga umahiri
katika ufundishaji wa dhana ya vipimo vya muda, urefu, uzito pamoja na ujazo.
Vipimo ni matumizi ya
namba katika vitu au matukio ukilinganisha na muda, urefu, uzito na ujazo
tofautitofauti. Dhana ya vipimo hujitokeza katika shughuli mbalimbali
tunazozifanya. Vipimo vinajitokeza katika ushonaji wa nguo ambapo ni lazima
fundi akupime, katika ujenzi ambapo hupima eneo la kujenga au upimaji wa uzito
na ujazo wa bidhaa mbalimbali. Kutokana na msingi huo, ni dhahiri kuwa dhana ya
vipimo ni muhimu sana katika maisha yetu. Ili uwe mwalimu mahiri katika
ufundishaji wa dhana hii unashauriwa kutumia vifaa au zana halisi pamoja na
mazingira yanayokuzunguka.
Kuna aina mbili za
vipimo ambavyo ni vipimo rasmi na vipimo
visivyo rasmi. Moja ya kipimo kisicho
rasmi ni wadi. Kipimo hiki kinatumika kukadiria urefu kwa kutumia mikono au
kutumia hatua za miguu kukadiria urefu wa shamba au eneo. Pia kuna utumiaji wa
makopo kukadiria ujazo wa vitu kama maji na vyakula. Vilevile kutumia muonekano
wa jua, mwezi au kuweka alama fulani kukadiria muda. Aina ya pili ni vipimo rasmi (vipimo vya
metriki) ambavyo vinajumuisha vipimo vya urefu, uzito, ujazo na jotoridi.
Katika moduli hii tutajifunza zaidi
kutambua vipimo visivyo rasmi kulingana na ngazi ya mwanafunzi
anayehusika.
Dhana ya matukio ya muda
Unaweza kuyabainisha
matukio yanayotokea katika nyakati tofauti kwa siku kwa kuoanisha picha au
michoro na tukio au muda ambao tukio limetokea
katika siku kama vile asubuhi, mchana, jioni au usiku.
Dhana ya urefu
Urefu
ni umbali kutoka nukta moja hadi nyingine.
Umbali huu unaweza kuoneshwa kwa mstari wa wima, ulalo au kwa
mzunguko. Pima urefu wa mwenzako na yeye
apime urefu wako, linganisha kisha andika matokeo katika jedwali hili. Chunguza
umbali kutoka nyumbani kwako hadi shuleni, dukani au sokoni na kadhalika.
Dhana ya ukaribu na
umbali

Vitendo vifuatavyo vinaweza kukusaidia katika kumjengea
mwanafunzi dhana ya ukaribu na umbali. i. Bainisha uhusiano wa karibu na wa
mbali kati ya mwanafunzi mmoja na mwingine. ii. Linganisha vitu vilivyo karibu
na vilivyo mbali katika mazingira ya shule kwa mfano madarasa, kengele na
mlingoti wa bendera ya shule.
Dhana ya kutambua uzito
Mambo
ya kuzingatia wakati wa ujifunzaji wa
dhana ya kutambua uzito:
i.
Kulinganisha
vitu vyepesi na vizito ili kupata tofauti.
ii.
Kulinganisha uzito wa vitu viwili vya aina
moja.
iii.
Kulinganisha uzito wa vitu viwili vya aina
tofauti.
Dhana ya ujazo
Dhana
ya ujazo inafundishwa kwa kutumia vitu vyenye nafasi, mfano chupa, debe, ndoo
zenye ukubwa tofauti na vimiminika mfano maji.
Ili uweze kufanya vizuri katika kuhusianisha dhana ya ujazo na maisha,
tumia vitu halisi na shughuli ambazo zinafanyika kila siku. Watu hufanya kazi
mbalimbali zinazohusu ujazo katika maisha yao ya kila siku; kwa mfano kujaza
maji katika vyombo. Ujazo upo katika matumizi yetu ya kila siku. Unapofundisha
dhana hii jaza maji kwenye vyombo viwili vyenye ujazo tofauti mbele ya
wanafunzi ili walinganishe na kubaini kuwa chombo kidogo hubeba maji kidogo
wakati chombo kikubwa hubeba maji mengi. Endelea kufanya vitendo vingine vya
ufundishaji wa dhana ya ujazo ili kuimarisha maarifa katika dhana hii ya ujazo.
Sura ya Tano
Kutambua maumbo
Karibu katika sura hii
inayohusu kutambua maumbo ambayo inalenga kukujengea umahiri katika kumfundisha
mwanafunzi kuyatambua maumbo kwa ufanisi. Baada ya kujifunza maudhui ya sura
hii utakuwa umejenga uwezo wa kufundisha dhana ya maumbo kwa ufanisi zaidi.


Sura ya Sita
Kukusanya na kuorodhesha vitu
Karibu katika sura hii
inayohusu kukusanya na kuorodhesha vitu. Baada ya kumaliza kujifunza dhana hii
utakuwa mahiri katika kufundisha dhana ya kukusanya, kuchambua, kulinganisha,
kutofautisha na kuwasilisha vitu.
Uchambuzi wa
vitu
Uchambuzi wa vitu ni
hatua ya ukusanyaji, upitiaji, upangaji na uwasilishaji wa data katika matumizi
ya taarifa. Dhana hii inamsaidia mwanafunzi kuona, kufafanua na kutofautisha
vitu au matukio na uhusiano wake. Pia, inamsaidia kutengeneza uhusiano au
muunganiko kati ya namba na maisha halisi ya kawaida.
Chunguza kielelezo
kinachoonesha aina za matunda na idadi ya wanafunzi :

Hatua za kuchambua vitu
Katika
kuchambua vitu ni muhimu kuzingatia hatua zifuatazo: Ukusanyaji, upitiaji,
upangaji na uwasilishaji wa taarifa. Katika vitendo vya ufundishaji unaweza
kukusanya vitu mbalimbali kama vile makasha, vibao, vihesabio, chupa za maji na
kadhalika, na baada ya hapo unaweza kuvipitia na kuvipanga na kisha kufanya
uwasilishaji wa taarifa hiyo.









Comments
Post a Comment