WIMBO WA SHUKURANI by Joakim chawe
Wimbo: Ushukuriwe Mungu Mtunzi: Joakim Chawe Sauti: Joakim Chawe Booking: 0754465961 Kwanza namshukuru Mungu, Aliyenifikisha hapa, Aliyenipa mi kibali, na kunifanya kuwa mshindi, Aliyenipa afya tele, Nakufanya niwe hodari, Ameondoa aibu, ameweka misingi ya haki, Kwake Bwana nasimama Ndiye mwamba Ni salama Ndie mwamba Ni salama kwake Bwana nasimama. Hakuna aliyedhani, kwamba leo tungekuwa hapa, Kila siku ilikuwa kulia, machozi hayakukauka, Hatukujua kesho yetu, Maana ya Jana tu yalitushinda, Ifikapo mapambazuko badala ya kufurahi, Tulilia Mana tuliona Ni afadhari ya Jana Mapambazuko yalipofika Tulijiuliza Ni wapi tule, ili angalau tusogeze siku Kwake Bwana nasimama Ndiye mwamba Ni salama ndiye mwamba Ni salama kwake Bwana nasimama. Ninasema Asante Bwana, Sitachoka kusema Asante Maana wewe Ni Mungu wangu Ulofanya mbingu na nchi... Habari wanafuns kwa majina naitwa Joakim, Mimi...