WIMBO WA SHUKURANI by Joakim chawe

 Wimbo: Ushukuriwe Mungu

        Mtunzi: Joakim Chawe

         Sauti: Joakim Chawe

         Booking: 0754465961

Kwanza namshukuru Mungu,

Aliyenifikisha hapa,

Aliyenipa mi kibali, na kunifanya kuwa mshindi,

Aliyenipa afya tele,

Nakufanya niwe hodari, 

Ameondoa aibu, ameweka misingi ya haki,

Kwake Bwana nasimama

Ndiye mwamba Ni salama

Ndie mwamba Ni salama kwake Bwana nasimama.



Hakuna aliyedhani, kwamba leo tungekuwa hapa,

Kila siku ilikuwa kulia, machozi hayakukauka,

Hatukujua kesho yetu, 

Maana ya Jana tu yalitushinda,

Ifikapo mapambazuko badala ya kufurahi,

Tulilia Mana tuliona Ni afadhari ya Jana

Mapambazuko yalipofika

Tulijiuliza Ni wapi tule,

ili angalau tusogeze siku

Kwake Bwana nasimama

Ndiye mwamba Ni salama

ndiye mwamba Ni salama kwake Bwana nasimama.



Ninasema Asante Bwana,

Sitachoka kusema Asante

Maana wewe Ni Mungu wangu

Ulofanya mbingu na nchi...



Habari wanafuns kwa majina naitwa Joakim,

Mimi niwandishi wa vitabu na makala mbalimbali za kitaaluma kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka kidato Cha sita.


Pia Ni mtunzi na mwandishi wa nyimbo, mashairi aina zote, simulizi, visa na Mikasa.


Unaweza kujifunza zaidi kupitia YouTube channel kwa jina la Joakim work Production

na WhatsApp namba: 0754465961

tellegram:@joakimworkproduction255


Asante see you at the top.



Comments

Popular posts from this blog

AKILI YA MWANADAMU