Mfalme masikini full episode
MFALME MASIKINI
By: Joakim artwork production
Simu: 0754465961whatsapp
Telegram: @joakimworkproduction255
Twitter: @joakim_chawe
YouTube: Joakim work Production
Katika himaya ya emperor katika miaka ya nyuma kidogo alikuwepo MFALME mmoja aliejulikana kwa jina la King Beaz. Alikuwa ni mfalme wa kwanza kushangaza ulimwengu, mbali na kwamba ufalme ulirithishwa lakini zilikuwepo sifa kadha wa kadha za yeye kuwekwa kwenye kiti kitukufu cha Cha ufalme Kama vile; hadhi, umri, Mali nyingi, majeshi ya kutosha na kadhalika. Kwa mfalme huyu ilikuwa Ni tofauti kabisa ambaye yeye alikuwa katika hali ya chini ya kiuchumi, umri mdogo na jeshi lake lilitumia silaha duni Kama vile fimbo na marungu. Licha ya hivyo himaya ya mfalme huyu ilikuwa na amani, mshikamano, na Uhuru wa kutosha, Jambo lililokuwa linawashangaza wafalme wengine duniani.
Joakim work Production Ni waandishi wa vitabu na makala mbalimbali za kitaaluma kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita. Pia msimu huu wa mwisho wa semister tunatoa punguzo kubwa kwa makala za wanachuo na wahitimu wa vyuo vikuu nchini iitwayo 'JIFUNZE NAMNA YA KUJITENGENEZEA CONNECTION KATIKA MAISHA YAKO/ LEARN HOW TO MAKE YOUR SELF CONNECTION IN YOUR LIFE'
Je, wazijua njia zaidi ya saba za kujitengenezea connection katika maisha yako? Makala hii itakuwa msaada kwako.
Mawasiliano:0754465961 WhatsApp
Email: joakimworkproduction@gmail.com
Licha ya umasikini aliokuwa nao mfalme Beaz lakini aliaminiwa na wananchi wake kuwa mtatuzi wa matatizo mbalimbali yanayotokea kwenye himaya yake Kama vile matatizo ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, na kijamii, najua Ni ngumu kuamini hapo.
Ndani ya kipindi kifupi toka mfalme huyu aingie kwenye madarakani alipendwa mno na wananchi wake na umaarufu wake ukasambaa sana katika mataifa makubwa. Wafalme wengi walikwenda katika himaya ya emperor kujifunza kwa mfalme huyu, walishangaa mno kuona hali Kama ile ya mfalme Beaz; hatujawahi kutokea duniani kwa ujumla alikuwa tofauti kabisa na wafalme wengine walikuwepo barani Afrika na duniani kwa ujumla kwani alilala juu ya kitanda kilichotengenezwa kwa ngozi Kama wananchi wake Jambo lililokuwa tofauti na wafalme wengine duniani, ambao wao hufanya juu chini, pembeni (kulia na kushoto) ili wawe na hadhi kubwa za kimaisha kuliko wananchi wao.
Siku moja wafalme wakubwa duniani walifanya ziara kwenye himaya ya emperor, bila kinyongo mfalme aliwapokea na akawa karibisha kabla hawajafika kwenye lango kuu aliwongoza kuzunguka mipaka yote ya himaya yake na kuwaonesha mandhari mbalimbali za kuvutia kweny himaya yake. Baadaye wafalme wale walianza kuchoka kutokana na safari ndefu, mfalme akaamuru Askari wake wafanye mawindo ya kuwakamata swala punde si punde swala watatu wakaletwa, haraka kazi ya kuwachuna ikaanza na baada ya swala wote wakabanikwa, nusu saa baadaye kitoweo kikawa tayari aliwakaribisha wafalme wakala wakapata nguvu za kuendelea na safari ya kurudi kwa kwa mfalme Beaz.
Ilipofika usiku ilikuwa ni baridi kidogo hivyo ikawalazimu wafalme wavae nguo nzito za kujikinga na baridi. Wafalme wale walitamani sana kujua Siri ya mfalme Beaz ya kuongoza watu katika hali ya umasikini wake mfalme akasema;
"Kuongoza watu ni kazi nyepesi sana na Ni kazi moja ngumu mno" akakohoa kidogo Kisha akasema, " punde si punde hali itabadilika hapa, naomba wote naomba wote kuanzia sasa tuvue mavazi yetu ya kujikinga maana joto litakuwepo"
Basi wote wakavua mavazi yao. Mfalme akatikisa kichwa ishara ya kuonesha kuridhika.
Alipopepesa macho yake aligundua kuwa Kuna wafalme kadhaa ambao wao hawakuvua mavazi yao ya baridi. Akasema;
"Bila maono hakuna uongozi, hakuna uongozi utakaosimama Kama hakuna maono..." Mfalme akaendelea, ndugu msomaji hapa kila swali atakalouliza swali wewe utajibu " Ni wewe" ukosaidiana na wafalme waliokwenda kujifunza kwa mfalme.
1.Mfalme: Ni nani aliyewaongoza ninyi toka mnafika?
w
Wote: "Ni wewe"
2.Mfalme: Ni nani aliyewaamuru Askari watafute kitoweo?
wote: "Ni wewe"
3. Mfalme: Ni nani aliyewapa chakula?
Wote:____________________
4. Ni nani aliyewaamuru mvue mavazi yenu?
Wote:_______________________
5. Mfalme: Ni nani aliyewakusanya wafalme wote duniani?
Wote:__________________________
Kwahiyo jibu likabaki Niwewe,Niwewe, Niwewe________ mpaka kikao kilipokwisha.
Wafalme kusikia hivyo wakatoa mavazi yao ya kifalme, mavazi yenye thamani yalioundwa kwa dhahabu na Vito vya thamani, wakaweka chini fedha na silaha zao ,wakamshukuru sana mfalme, hawakuamini walichoambiwa na mfalme Beaz;kutoka hapo mfalme akawa tajiri kwa ufalme wa matajiri wengine, himaya yake ikabadilika badala ya nyumba kujengwa kwa tope pamoja na miti zikajengwa kwa kwa dhahabu na Vito vya thamani. Hapo ndipo mfalme MASIKINI alipowaongoza wafalme matajiri kwa muda mchache; wafalme hawakuacha kumtembelea king Beaz hata yeye aliitwa kwenda nchi za nje.
Ninachotaka kusema hapa; Ni kweli Hali ngumu za maisha zinawatesa watu, maono ni kitu muhimu sana katika maisha. Jifunze kuishi vizuri na watu, shirikiana nao katika hali zote (huzuni na furaha) au kupata na kukosa.
Na mwisho nipende kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Samia S. Hassan kwa uongozi wake, najua salamu zitamfikia kwa muda na wakati wowote. Haya no maneno yangu kutoka katika vilindi vya moyo wangu;
" Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Samia S. Hassan, mimi nisiyestahili kusimama mbele yako au kuchukua kalamu na kuandika ujumbe huu kutokana na hali yangu duni ya kimaisha na umri wangu kuwa mdogo. Lakini nakupongeza ( mimi kama mwananchi wako) kwa kazi yako kubwa ya kuwaongoza watanzania
,Sipo peke yangu ninaekushukuru, nyuma yangu wapo watu wengi wanaokushukuru japokuwa hawaonekani.
Hatakama kazi uliopewa ni kubwa mno au ni ngumu kwa kiasi gani, tambua kuwa umeaminiwa na wengi kuwa wewe unaweza kubadili maisha ya watanzania kutokana na maono yako.
Mh. Rais we Jamhuri ya muungano wa Tanzania sisi tunaitambua kazi yako na tunakuhahikikishia tutakuwa pamoja na wewe mpaka kufikia kilele cha mafanikio ya nchi yetu. Sijui nini nimewaza mpaka kuandika ujumbe huu kwako. Kwa maombi ya watanzania tunaamini kuwa tutafika tu.
Tunakuamini na tupo pamoja na wewe.
Kwa niaba ya wote wanaotambua kazi kubwa ulionayo juu ya watanzania, mimi naitwa Joakim Chawe."
Asante.
Unaweza kupata simulizi hii kupitia whatsapp namba 0754465961 au kupitia Email: joakimworkproduction@gmail.com/Joakimworkproduction255@yahoo.com kwa shilingi 500 tu! Follow ukurasa wetu wa Twitter: @joakim_chawe
#NAKUSANYA MAONI
SIMULIZI INAYOFUATA INAITWA "MEZA YA MWANDISHI"
weka oda yako mapema kwa kupiga simu namba- 0754465961 au njoo WhatsApp Kisha andika " Artwork production, simulizi" Kisha utarushiwa simulizi yote.
Artwork production pata burudani kamili hapa.
Comments
Post a Comment