MASAA MATATU ya hukumu
MASAA MATATU ZA HUKUMU
(Three hours for Judgement)
Safari Ya Kifo
Joakim Chawe
+255 754 465 961
Hiki ni kisa kinachofahamika na waliowengi na ni moja kati ya visa vinavyotokea ulimwemguni Ila no mgumu sana kumsimulia mtu mpaka akakuelewa. Inahitaji nguvu kubwa ya kiimani ama ya kufananisha kisa hiki na ushirikina.
Nina imani kwamba kisa hiki kitakuwa na ujumbe mkubwa kwa wasomaji wengi.
Ni kisa kinacho muhusu kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Emmanuel ambae alikuwa na umri wa miaka ipatayo 25 na kwa kijana huyu ambae alikuwa na umri wa kuoa na alikuwa chini ya imani ya kikristo, Twende sambamba tufuatilie kisa mpaka mwisho wa kisa hiki.
MASAA MATATU YA HUKUMU
¶ Imefikia kipindi Cha Mimi kuwa na mwenza, nifanye nini ili nimpate mwenza sahihi katika maisha yangu?
¶ Alafu wewe si unasali, kinachokushinda kufanya maamuzi ni nini?
MASAA MATATU YA HUKUMU...1
Kwa majina naitwa Emmanuel Mdopa, nasimulia kisa hiki ambacho mpaka sasa huwa najiuliza kwanini nipo hai? Ni kisa ambacho kilipanga kuyamaliza maisha yangu. Laiti kama ningelikufa huo ndio ungekuwa mwisho wa historia yangu duniani, jina langu lingesahaulika na pengine watu wasimgeuona mwili wangu kabisa kutokana na mazingira ambayo nilikuwepo, mazingira yasio julikana.
Ilikuwa jumapili tulivu majira ya saa saba mchana hivi nikiwa nimetoka kanisani huku nikiwa nimegubikwa na mawazo ya kutaka kuoa na wakati huo nilikuwa bado nakaa kwa wazazi wangu na suala la kujenga au kupanga kwangu lilikuwa kitendawili kutokana na uhaba wa fedha ukizingatia ni mwaka mmoja ulikuwa umepita toka nitoke kuhitimu masomo yangu ya chuo kikuu.
Nikiwa njiani niliwaza namna mbalimbali za kupata mke mzuri katika maisha yangu lakini nikiwa katika dimbwi Hilo la mawazo nikakumbuka kuwa Mimi Sina pesa jambo lililonikatisha tamaa.
Nilifika nyumbani nikaweka kibegi changu nimachobebeaga biblia kisha nikaelekea ofisini, nikiwa maeneo ya ofisi ambayo ilikuwa karibu kabisa na barabara, upande wa chini nikamuona dada mmoja akinipa ishara ya kuniita huku akiongea na simu, nikaenda nilipomkaribia Cha ajabu aliendelea kuongea na simu yake ilabidi nimsubiri mpaka amalize mazungumzo yake, alichukua Kama nusu saa hivi alipomaliza alinishika mkono ishara ya kunisalimia huku akijisemesha
"pole kaka nimekuchelewesha"
aliongea yule dada huku akiweka simu yake kwenye pochi lake.
Nilikwambia kuwa asijali lakini moyoni nilimchukia kwa kitendo alichokifanya.
Kiukweli alikuwa ni mtu alieomekana kunichangamkia sana Kama ananifahamu vile Ila kiukweli hata mimi nilikuwa nikijiuliza alishawahi kuniona wapi?
Muda si mrefu aliingiza mkono wake kwenye pochi lake na kutoa business card yake (kadi ya biashara) huku akisema "samahani kaka najua nimekukosea kwa kukupotezea muda wako, naomba uchukue kadi hii muda utakaopata muda naomba unitafute Kuna Mambo nataka kujadiliana na wewe"
"bila shida" niliongea huku nikiwa Kama nimefurahi Kisha yule dada akawa anaondoka huku akinisisitiza nimtafute kwa njia ya simu. Nilikubaliana nae Kisha nikageuka kuelekea ofisini ili kuendelea na kazi zangu. Kabla sijapiga hatua nyingi nilimsikia yule dada akiita "we kaka" nikageuka Kisha nikajishitukia kumbe alikuwa anaongea na simu nililitambua Hilo baada ya kuona simu kubwa ikiwa kwenye sikio lake la upande wa kushoto akiwa ameshikilia kwa mkono wake. Nikiwa katika
Comments
Post a Comment